Kiu ya Mabadiliko
Mchapishaji
Lantern - George Cleopa Mapunjo
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Kiu ya Mabadiliko ni tamthiliya yenye kubainisha sauti kali ya utetezi kwa wavujajasho wanaonyanyaswa, kuonewa, kudharauliwa na kunyonywa nguvu zao. Ni tamthiliya yenye kuuzindua umma uliogubikwa na giza nene na hivyo kuhitaji mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii dhidi ya tabaka tawala. Kupitia tamthiliya hii, mimi, wewe, wao na wengine wengi wanaitaji mabadiliko. Tumia nafasi yako kupigania mabadiliko.
Vitabu vingine vya Mwandishi ni Siri ya Mtoto ajuaye Mama, Pasua Kichwa na Tujipange Watupange? ambavyo ni vya Mashairi na Mtoto wa Mtawala.