Uchochoro wa Tanzanite
Mchapishaji
Ape Network
Lugha
Swahili
MAELEZO YA KITABU
Alex, afisa usalama, anapenyezwa Wizara ya Madini kufichua kinachoendelea katika upotevu tata wa mapato ya Taifa ndani ya biashara ya madini ya Tanzanite. Anaambulia taarifa kiduchu.
Kitendawili kinabaki, ni kina nani wanahusika na biashara hii haramu kimataifa? Kutegua kitendawili, Alex anaondolewa wizarani na kutumwa kwenye misheni ya siri. Lengo ni kufichua mtandao ili hatimaye Taifa lipate kuudhibiti Uchochoro mzima wa Tanzanite. Alex anakutana na mauaji, usaliti, visasi na ukatili kutoka kwa magenge ya wahalifu ya kimataifa.