
MAELEZO YA KITABU
KUFIKIRIKA ni riwaya fupi inayotumia mandhari ya kufikirika lakini lakini maudhui yake yanasadifu maisha ya jamii za kiafrika kwa sehemu kubwa. Kwa kawaida ndoa katika jamii za kiafrika hazipo kwa ajili ya mume na mke kuishi pamoja tu bali ni kupata watoto. Watoto ndio furaha na faraja ya wanandoa. Kutokanana Imani hiyo, ndoa ya mfalme na malkia wa kufikirika inagubikwa na wingu la huzuni kuu kutokana na wao kuandamwa na ugumba na utasa. Kwa huzuni kuu, mfalme anaamua kumshirikisha waziri wake mkuu kuhusu kadhia hiyo ambapo uamuzi unafikiwa kuwa mfalme na malkia waaguliwe. Nchi ya kufikitika imebarikiwa sana kuwa na waganga wengi na wa aina nyingi ambao walipaswa kuwatibia mfalme na malkia ugumba na utasa wao. Kulikuwapo na waganga wa mizizi, wakafara, mazinguo, hirizi, mashetani na utabiri. Kwa bahati mbaya, uchaguzi wa kundi lipi la uganga lianze kuwatibia mfalme na malkia lilikosewa. Badala ya kundi la utabiri kuanza yalianza makundi mengine matano ambayo hayakufaulu kuleta tiba mujarabu kwa mfalme na malkia Zaidi ya kuleta maafa makubwa. Misitu, wanyama, mifugo na vyakula viliteketezwa bure bilashi. Hili lilikuwa ni jambo baya na la kusikitisha kabisa. Laiti bahati ya kuchaguliwa kuwa kundi la kwanza la matibabu ya mfalme na malkia ingaliangukia kundi la utabiri mali za nchi ya kufikirika zingali okoka au maangamizi yake yangalikuwa madogo sana. Utabiri ulionesha wanandoa hawa wangepata mtoto baada ya muda Fulani. Na mtoto huyo angezaliwa baada ya miezi tisa ama kumi na angekuwa wa kiume. Hata hivyo mtoto huyo atapata maradhi baada ya kufikisha umri wa miaka kumi na tiba yake itakuwa kufanya kafara la damu za watu wawili vinginevyo mtoto atakufa. Na wahanga hao lazima wawe mwerevu na mjinga. Kafara hii lilikifanywa mtoto ataishi Mkuu wa kundi la utabiri alikuwa utubora ujinga hasara na ndiye aliyetoa utabiri wote. Jambo la kushangaza ni kuwa mmoja wa wahanga wa kafara la damu alikuwa ni yeye mwenyewe. Mtoto wa mfalme anafikisha miaka kumi na anaumwa. Ni kigezo gani kitatumika kuwapata watu hawa yaani wahanga wa kafara la damu, mwerevu na mjinga? Je, watachinjwa? Je, mtoto atapona? Ungana na mwandishi wako Shaaban Robert hadi mwisho ilikujua yapi yatajiri.