PENINA MUHANDO

BIOGRAPHY




Nguzo Mama

Penina Muhando (Pia Penina Mlama) ni mwandishi mbobevu na mwanazuoni wa Kiswahili hususan katika utanzu wa tamthiliya. Ameandika tamthiliya kama vile Heshima Yangu (1974), Pambo (1975), Lina Ubani (1984) na Mitumba Ndui (1989).


  • Published : February 1, 2022

Lina Ubani

No Description


  • Published : January 5, 2023

Pambo

Pambo ni kitabu kinachotoa mfano kamili wa dhamira mgongano unaowapata baadhi ya vijana wetu. Mwandishi ametumia mfano wa kijana Pambo kueleza tatizo hili kwa namna inayovutia.


  • Published : January 5, 2023

Harakati za Ukombozi

Katika nchi moja ya Afrika, watu wamehangaika kudai uhuru na wameupata. Ila punde wanagundua kuwa wenye dhamana ya kuunda ukombozi wamejiweka mbele katika kufaidi matunda ya ukombozi


  • Published : November 20, 2024

Hatia

Binti Cheja anapelekwa mjini na wazazi wake kufanya kazi kwa Sembuli – mwanakijiji mwenzao. Huko mjini Cheja anakutana na mwanamume, wanafanya jambo na Cheja anapata mimba! Kinyume na matarajio ya Cheja, Juma hana mpango wowote naye wala hataki kusikia habari ya huo mzigo Cheja alionao.


  • Published : November 20, 2024

Hidaya ya Penina Muhando Volume One

Maandishi ni njia muhimu ya kuhifadhi maarifa, taarifa na utamaduni wa watu. Kupitia maandishi, simulizi za matukio, hekima na tajiriba za jamii hunaswa na kufanywa kuishi milele na hivyo kutegua kitendawili cha ukomo ambao kifo huleta kwenye uendelevu wa mambo.


  • Published : November 20, 2024

Hidaya ya Penina Muhando Volume Two

Maandishi ni njia muhimu ya kuhifadhi maarifa, taarifa na utamaduni wa watu. Kupitia maandishi, simulizi za matukio, hekima na tajiriba za jamii hunaswa na kufanywa kuishi milele na hivyo kutegua kitendawili cha ukomo ambao kifo huleta kwenye uendelevu wa mambo


  • Published : November 20, 2024

Lina Ubani

Jamii inakosa usawa na viongozi waliopewa dhamana wanakuwa mstari wa mbele kuharibu badala ya kujenga. Watawala hawashauriki na maamuzi yao yanatengeneza njia itakayoielekeza nchi korongoni.


  • Published : November 20, 2024

Pambo

Hali ya Pambo inabadilika ghafla, anaanza kufanya mambo yanayoashiria kuwa ana changamoto kiakili.


  • Published : November 20, 2024

Talaka Si Mke Wangu

Migogoro katika familia inazua hasira na hasira inazaa talaka. “...Ee chukua... Talaka si mke wangu... Nenda na mimi nipate kutulia roho...” Hivyo ndivyo mume anavyomtaliki mkewe.


  • Published : November 20, 2024

Tambueni Haki Zetu

Raia wa nchi huru wanajikuta katika hatari ya kutawaliwa na wageni ambao wao wenyewe waliwakaribisha. Uhuru na amani yao imeingiliwa na kuna hatihati ya kuupoteza.


  • Published : November 20, 2024

Kodi

Maisha yamekuwa na changamoto nyingi kwa watu wengi. Watoto wanafukuzwa shule, mke na mume hawaelewani na wengine wanafikia kuogopa hata kukaa nyumbani kwao, watoto na wazazi wanagombana, raia wanawalaumu viongozi wao...


  • Published : November 21, 2024


No award found

Ask Penina Muhando anything

Contact Form