
BOOK OVERVIEW
SIKU YA WATENZI WOTE ni riwaya ya kijamii inayojadili maisha ya wanadamu namna wanavyohusiana wao kwa wao na pia baina yao wao na Mungu. Ni riwaya inayozungukia kipindi cha mabadiliko katika nchi ya Tanganyika mara tu baada ya uhuru. Mabadiliko hayo yamegusia Nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Pamoja na mabadiliko hayo hasa ya kisiasa, tabaka la wenyenacho linaendeleza dhuluma, ufisadi, ukatili, uonevu na maovu mengine na kuwaacha watu wa tabaka la chini katika njaa kali, umasikini uliokithiri, makazi duni na kukata tamaa.
Mwandishi amewatumia wahusika kadhaa wenye mapenzi bora ambao wamejitolea kuwasaidia watu wenye maisha duni. Baadhi yao ni Binti Akili na Ayubu. Riwaya hii imegusia pia imani ya binadamu katika dini. Mwandishi anasema, “Utatuzi wa mashaka ya ulimwengu ulikuwa katika maungano ya imani yaliyoletwa na umoja wa dini”
Shaaban Robert ametoa mawazo yake na imani na mtazamo wake kuhusu maisha ya kila siku ya mwanadamu. Riwaya hii nzuri kwa yeyote anayependa kujua historia na maisha ya Watanganyika hasa wakazi wa Dar es Salaam mara tu baada ya kupatikana kwa uhuru.