Mapenzi Yamelogwa
Publisher
Lantern-E-Books
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 18, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

Riwaya hii niliitunga mwaka 2002 wakati huo nikimuuguza marehemu mama yangu Bi. Hawa Ally Rwazihonda aliyefariki dunia Desemba 24’ 2002. Mola amlaze mahala pema peponi. Wakati nikiitunga nilidhamiria itoke katika gazeti la Ijumaa na baadae Mwananchi, lakini kutokana na sababu mbalimbali haikuweza kutumika. Kutoka hapo nimekaa na simulizi hii kwa takribani miaka kumi na mbili mpaka ilipokuja kuonwa na ndugu yangu katika fani Kaka Kelvin Emmanuel Gaspar Mponda ndipo aliponihamasisha tena kuitoa riwaya hii kwa jamii kwa maelezo kwamba ilikuwa ni hazina kubwa. Namshukuru sana kwa hilo na kwa mengi ambayo ameyafanya katika kuhakikisha riwaya hii inakuwa katika ubora ilionao. Lakini ni ukweli kuwa kazi hii mpaka kufika mikononi mwako, juhudi mbalimbali zimefanyika ambazo kiukweli hazikuwa haba. Kwa uchache ningependa kuwataja baadhi walionisaidia kwa hali na mali. Kwanza ni baba yangu mzazi Mzee Msafiri Wamaywa kwa kunipa elimu na miongozo iliyoniwezesha mimi leo kuwa kama nilivyo, pili ni baba mlezi, Mzee Stanley Mathew Kishindo na Mama Sophia Kishindo wa Kimara Kilungule; ni hawa walionipokea Dar es Salaam nikiwa sina mbele wala nyuma, wakanipa kila kitu, huku wakinilea katika namna ambayo hata watoto wao wa kuwazaa hawakuwatendea hivyo. Dhahabu Arts Group ambayo leo imeniajiri kama Katibu Mtendaji, ilizaliwa chini yao na wao walikuwa wafadhili wakuu. Nawapenda sana wazazi wangu na muendelee kujua kuwa mchango na msaada wenu kwangu ni mkubwa usio na kifani. Ahsanteni sana. Nimshukuru mke wangu Lulu J. Mandaro, mzazi mwenzangu Asia Khalifa kwa kuwa pamoja nami licha ya changamoto mbalimbali za kimaisha. Niwashukuru Ndugu zangu Abbas Said Mzeru, Peter Nicholaus Kibehi, Marco Tibasima, Kessa Mwambeleko, Mashaka Mkesso Gama, Frank John Mariki, Lupia Mashauri, Jackson Gembe na dada Emma J. Medda. Nawashukuru ndugu zangu katika fani kaka Hussein Issa Tuwa, kaka Ibrahim Marijani Gama, kaka George Iron Mosenya na mzee wangu Robert R. Mhangwa kwa msaada na ushirikiano mkubwa walionipa hasa katika kuboresha riwaya hii. Ahsanteni sana. Siwezi kuwasahau pia wapenzi wa simulizi zangu tangu nikiandikia majarida ya Bongo, Bantu, Tabasamu, Tunu na Tanua Comics. Pia magazeti ya Zeze, Mwananchi, Nipashe, Uhuru, Mzalendo, Ijumaa Wikienda na mengine mengi. Zaidi ni Mwalimu Msita (Hilda Yohana) ambaye alinipokea pale shule ya Msingi Kiezya, Kigoma mwaka 1991 akawa mtu wa awali kunifanya niweze kusoma na kuandika. Mengi niyafanyayo katika maandishi yalianzia kwake. Ahsante sana Mwalimu wangu. Kwa namna ya kipekee namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai, uwezo na kipawa hiki cha utunzi. Pamoja na kuniwezesha kukitoa kitabu hiki. Bila yeye mimi ni sifuri. Namshukuru sana. Zaidi ni kwa wanangu wapendwa Hawa Wamaywa, Msafiri Wamaywa na Johari Wamaywa ninawapenda sana. Naendelea kuwaasa kuwa dunia ni sehemu ya kupita tu. Timizeni wajibu wenu, msisahau ibada na fanyeni kila lililo jema ili mtakapoondoka duniani mchango wenu uweze kubaki kama kumbukumbu kwa vizazi na vizazi! Siwezi kuwasahau ndugu zangu Stallone Joyfully ‘Mtoto wa Ben R. Mtobwa’ kwa misaada yake isiyo na kifani kwangu, Brian Mshana na Mwamwingila Goima Peter kwa kunitoa kizani, Marco Tibasima na Abbas Mzeru. Kwa kweli ninayo orodha ndefu ya kuwashukuru ambayo siwezi kuimaliza katika ukurasa huu, itoshe tu kusema ndugu zangu wote wakiwemo shabiki zangu, ninawashukuru sana na Mungu awabariki. Amin.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review