Hatinafsi
Publisher
Uwaridi
Language
Swahili
BOOK OVERVIEW
Pumzi ya mwisho aliyoivuta mkiwa ilikuwa ndiomwanzo wa sokomoko kwa familiya aliyoiacha nyuma, Mwanamkuu, mama mjane wa watoto wanne anageuka kuwa kichwa cha familia. Mvanda, kaka wa marehemu anakuwa ni chui baada ya kujivua ngozi ya kondoo aliyokuwa amejivika.
Vuta n'kuvute ya Mwanamkuu na shemejiye inaacha athari na uchungu mkubwa kwa Mwanamkuu na watoto wake.
Mvanda anadhamiria kuisambaratisha kabisa familia ya marehemu kaka yake. Nafsi yake iliyojaa uchu na tamaa inampelekea kufanya mambo kwa kuipendelea nafsi yake tu.
Je Mvanda atafanikiwa katika hili, na je Mwanamkuu atakabiliana naye vipi kuinusuru familia yake?