Almasi za Afrika
Publisher
Mbiu Press
Language
Swahili

Rent This Book

Expires on August 17, 2025

TSh 2,000/=

Choose Option

BOOK OVERVIEW

ALMASI ZA AFRIKA Ni mkusanyiko wa mashairi, riwaya na tenzi nyingi zenye wingi wa hekima na maadili mema kuhusu maisha ya binadamu. Mwandishi Shaaban Robert anayatazama maisha katika Nyanja zote kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Kwa ujumla ameyatafakari maisha na kuyaona kuwa yamejaa mambo mengi, mema na mabaya.

 

Almasi za Afrika” ni lugha ya picha inayoashiria vitu vya thamani kubwa kama ilivyo madini ya almasi. Afrika   ni bara tajiri katika tamaduni zake na pia utawala wake. Kazi nyingi za mwandishi huyu zimejaa nasaha nyingi sana lakini kwa bahati mbaya hazijaweza kuwafikia watu wengine wa ulimwengu ndani na nje ya Afrika. Kupitia kazi zake Utubora mkulima, Masomo yenye Adili, Kufikirika, Kusadikika, Adili na Nduguze, Insha na Mashairi, Pambo la Lugha, Mwafrika Aimba, Siku ya Watenzi Wote na Ashiki Kitabu Hiki, mwandishi ameweka wazi almasi hizi kwa kila mtu kujichotea hekima hizo.

 

Kazi hizi ni tunu kwa kila mmoja. Mwandishi ametimiza wajibu wake kikamilifu. Ndani ya vitabu hivi kwa maelekezo ya namna ya kumshukuru Mungu, kuwa na kiasi katika mambo yote tutendayo, uhusiano mwema baina yetu na kubwa zaidi kujivunia lugha yetu ya Kiswahili. Mwandishi analinganisha mahali kama vile vazi linavyompamba mtu. Anasema kuwa Lugha hupambwa zaidi na mashairi.

COMMUNITY REVIEWS

There are no reviews for this book yet

Write a Review